Event Date: 
14-10-2021

Wenza wa wachungaji wa KKKT Sharika za Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) wametoa shukrani katika Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront Cathedral kama sehemu ya kuadhimisha miaka nane tangu kuanzishwa kwa vicoba ambayo mpaka sasa ina akiba ya takriban Tsh 400,000,000/-. Pia vicoba hiyo hivi karibuni imechaguliwa kuwa vicoba bora katika nyanja ya uwekezaji nchini Tanzania.

Mama Anna Mzinga, M/Kiti wa vicoba hiyo inayomilikiwa na wenza wa wachungaji ametoa shukrani kwa Uongozi wa Dayosisi, Sharika zote za DMP pamoja na Uongozi wa Usharika wa Kanisa Kuu AZF kwa kuendelea kuwaunga mkono katika kipindi chote tangu vicoba hiyo kuanzishwa.

“Malengo ya Umoja huu pamoja na Vicoba hii ni kutuweka pamoja, kuwekeza na kuinuana kiuchumi. Tunatoa shukrani kwa wenza wetu ambao ni wachungaji kwa kuendelea kutuunga mkono ili kufanikisha malengo yetu, Mungu wabariki sana,” alisema Mama Anna Mzinga.

Ibada hiyo ya shukrani ambayo imefanyika Jumapili (10/10/2021) pia imehudhuriwa na Baba Askofu wa DMP, Dk Alex Malasusa akiambatana na Dean Chediel Lwiza pamoja na Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa AZF, Mchg Charles Mzinga.

Picha: Matukio mbalimbali katika picha wakati wa ibada ya shukrani

Angalia ibada hiyo AZANIAFRONT TV kupitia link hii hapa chini;

IBADA YA SHUKRANI - WENZA WA WACHUNGAJI DMP

-----------------------------------------------------------------------------------------

Ripoti hii imeandaliwa na; Paulin Paul