Date: 
24-01-2022
Reading: 
Wagalatia 2:11-14

Jumatatu asubuhi tarehe 24.01.2022

Wagalatia 2:11-14

11 Lakini Kefa alipokuja Antiokia, nalishindana naye uso kwa uso, kwa sababu alistahili hukumu.

12 Kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini walipokuja wao, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.

13 Na hao Wayahudi wengine wakajigeuza pamoja naye, hata na Barnaba pia akachukuliwa na unafiki wao.

14 Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?

Mungu anaondoa ubaguzi;

Mtume Paulo anamkemea Kefa kwa tabia ya kutenga baadhi ya watu wakati wa huduma yao. Kefa aliwashawishi wengi akiwemo Barnaba kuwa na tabia kama ya kwake, yaani kubagua watu. Katika mstari wa 14, Paulo anamkemea hadharani kwa tabia hii isiyompa Mungu utukufu.

Jamii tunayoishi inazo tabia hizi kwa baadhi yetu. Yupo anayebagua watu kwa sababu tu yeye ni wa daraja lingine kielimu, kiuchumi, hata kiimani! Lakini Yesu alikuja kwa ajili ya wote, na huu ndiyo mfano tunaoitwa kuufuata, yaani kukaa pamoja kama familia ya Mungu pasipo kubaguana.

Nakutakia wiki njema isiyo na ubaguzi.