Date: 
15-03-2021
Reading: 
Waebrania 9:1-10 (Hebrews 9:1-10)

JUMATATU TAHERE 15 MACHI 2021, ASUBUHI

Waebrania 9:1-10

1 Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia.
2 Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu.
3 Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu,
4 yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;
5 na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja.
6 Basi, vitu hivi vikiisha kutengenezwa hivyo, makuhani huingia katika hema hiyo ya kwanza daima, wakiyatimiza mambo ya ibada.
7 Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi za kutokujua za hao watu.
8 Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama;
9 ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye,
10 kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.

Yesu ni chakula cha uzima;

Ni habari ya maskani ya duniani na mbinguni kuhusu ibada. Tunaona jinsi  ibada ilivyokuwa hapo zamani, ambapo Kuhani alipanda madhabahuni, patakatifu, penye chetezo cha dhahabu na sanduku la Agano kufanya ibada. Zilikuwepo sadaka za kuteketezwa. Vyote hivyo vikishakuwepo, kuhani hufanya ibada.

Lakini baada ya Yesu kuja, aliye Kuhani mkuu, aliye mjumbe wa Agano jipya, ibada hufanyika kwa msingi wa damu yake iliyomwagika kwa ajili ya ondoleo la dhambi.

Hatutoi tena sadaka ya kuteketezwa, bali Yesu ndiye aliyekufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Tuishi maisha ya toba, ili damu ya Yesu itusafishe mioyo yetu, tuendelee kumwabudu Mungu aliye hai.

Nakutakia Juma jema lenye mafanikio.


MONDAY 15TH MARCH 2021, MORNING

HEBREWS 9 :1-10

The first promise that was made included rules for worship and a tent for worship here on earth. The first part of the tent was called the holy place, and a lampstand, a table, and the sacred loaves of bread were kept there.

Behind the curtain was the most holy place. The gold altar that was used for burning incense was in this holy place. The gold-covered sacred chest was also there, and inside it were three things. First, there was a gold jar filled with manna.[a] Then there was Aaron’s walking stick that sprouted.[b] Finally, there were the flat stones with the Ten Commandments written on them. On top of the chest were the glorious creatures with wings[c] opened out above the place of mercy.[d]

Now isn’t the time to go into detail about these things. But this is how everything was when the priests went each day into the first part of the tent to do their duties. However, only the high priest could go into the second part of the tent, and he went in only once a year. Each time he carried blood to offer for his sins and for any sins that the people had committed without meaning to.

All of this is the Holy Spirit’s way of saying that no one could enter the most holy place while the tent was still the place of worship. This also has a meaning for today. It shows that we cannot make our consciences clear by offering gifts and sacrifices. 10 These rules are merely about such things as eating and drinking and ceremonies for washing ourselves. And rules about physical things will last only until the time comes to change them for something better.

Read full chapter

Jesus is the bread of life;

It is the story of the earthly and heavenly tabernacle about worship. We see how the worship was in ancient times, where the Priest ascended the altar, the sanctuary, the golden censer and the Ark of the covenant to worship. There were burnt offerings. When all of this is done, the priest performs the ritual.

But after Jesus comes, who is the High Priest, the messenger of the New Testament, worship is performed on the basis of his blood shed for the remission of sins.

We no longer offer burnt offerings, but Jesus died for the sins of the world. Let us live a life of repentance, that the blood of Jesus may cleanse our hearts, and that we may continue to worship the living God.

I wish you a successful and prosperous week.