Date: 
21-01-2022
Reading: 
Waebrania 13:1-4

Ijumaa asubuhi tarehe 21.01.2022

Waebrania 13:1-4

1 Upendano wa ndugu na udumu.

2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.

3 Wakumbukeni hao waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; na hao wanaodhulumiwa, kwa vile ninyi nanyi mlivyo katika mwili.

4 Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.

Mungu hutakasa nyumba zetu;

Sura ya nne ya waraka kwa Waebrania ni maelekezo jinsi ya kuishi katika njia nyoofu. Mistari minne ya mwanzo tuliyosoma inatuelekeza kuwa na upendo, kukaribishana, kuwakumbuka wafungwa na wanaodhulumiwa, pia kuishi kwa uchaji katika ndoa. Ni msisitizo wa kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu.

Tusipoishi kwa kumfuata Yesu, hatuwezi kuwa mashuhuda wa imani yetu. Tunakuwa mashuhuda kwa kufuata maelekezo ya kuishi kwa kupendana na kila mmoja kumjali mwingine. Yesu anatuita kumfuata tukitenda mema, ili atakase nyumba zetu.

Ijumaa njema.