Date: 
25-01-2022
Reading: 
Waamuzi 2:20-23

Jumanne asubuhi tarehe 25.01.2022

Waamuzi 2:20-23

20 Basi hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili wamelihalifu agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu;

21 mimi nami tokea sasa sitalifukuza taifa mojawapo la hayo aliyoyaacha Yoshua alipokufa;

22 ili kwa njia ya hayo nipate kuwajaribu Israeli, kwamba wataishika njia ya Bwana kwenda katika njia hiyo, au sivyo.

23 Basi Bwana akawaacha mataifa yale, wala hakuwafukuza kwa upesi, wala hakuwatia katika mikono ya Yoshua.

Mungu anaondoa ubaguzi;

Mungu alikasirika kwa watu wake kumuasi, yaani kuiacha njia yake. Pamoja na kukasirika, hakuwafukuza mbele za uso wake, bali aliwapa nafasi ya kumrudia. Alionesha huruma yake.

Hata leo, Mungu hutupa nafasi ya kumrudia kwa njia ya toba. Hataki tuwe waovu, hatimaye kufa tukiwa dhambini. Mungu hufanya hivi kwa wote, akionesha hana ubaguzi. Tuitumie nafasi hii kuishi maisha ya toba, ili mwisho wetu uwe mwema katika Kristo. Siku njema.