Date: 
27-12-2016
Reading: 
Tues 27th Dec: Matthew 2:19-23 (NIV)

TUESDAY 27TH DECEMBER 2016 MORNING                

Matthew 2:19-23  New International Version (NIV)

The Return to Nazareth

19 After Herod died, an angel of the Lord appeared in a dream to Joseph in Egypt 20 and said, “Get up, take the child and his mother and go to the land of Israel, for those who were trying to take the child’s life are dead.”

21 So he got up, took the child and his mother and went to the land of Israel. 22 But when he heard that Archelaus was reigning in Judea in place of his father Herod, he was afraid to go there. Having been warned in a dream, he withdrew to the district of Galilee, 23 and he went and lived in a town called Nazareth. So was fulfilled what was said through the prophets, that he would be called a Nazarene.

God spoke to Joseph to guide him in his life. God spoke to him through and angel and through a dream to guide and warn him. Joseph was listening to God and he obeyed God.  God will mainly speak to us through His Word in the Bible and when we pray. Are we listening to God? Do we always obey Him?   

JUMANNE TAREHE 27 DISEMBA 2016 ASUBUHI                      

MATHAYO 2:19-23

19 Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, 
20 akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. 
21 Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli. 
22 Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya, 
23 akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.

Mungu aliongea na Yusufu kumwongoza na kumwonya. Mungu alitumia malaika na ndoto pia.  Yusufu alimsikiliza Mungu na alimtii. Mungu anaongea na sisi hasa wakati tunasoma  Neno lake (Biblia) na wakati wa maombi. Je! Tunamsikiliza na kumtii?