Date: 
01-12-2022
Reading: 
Sefania 1:8-17

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 01.12.2022

Sefania 1:8-17

[8]Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya BWANA, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni.

[9]Na katika siku ile nitawaadhibu hao wote warukao juu ya kizingiti, waijazao nyumba ya bwana wao udhalimu na udanganyifu.

[10]Na katika siku ile, asema BWANA kutakuwako sauti ya kilio kutoka lango la samaki, na mlio mkuu katika mtaa wa pili, na mshindo mkuu kutoka milimani.

[11]Haya! Lieni, ninyi mkaao katika Makteshi, maana wafanya biashara wote wameangamia; hao wote waliokuwa na mizigo ya fedha wamekatiliwa mbali.

[12]Kisha itakuwa wakati ule, nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.

[13]Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake.

[14]Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu; 

I karibu, nayo inafanya haraka sana; 

Naam, sauti ya siku ya BWANA; 

Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!

[15]Siku ile ni siku ya ghadhabu, 

Siku ya fadhaa na dhiki, 

Siku ya uharibifu na ukiwa, 

Siku ya giza na utusitusi, 

Siku ya mawingu na giza kuu,

[16]Siku ya tarumbeta na ya kamsa, 

Juu ya miji yenye maboma, 

Juu ya buruji zilizo ndefu sana.

[17]Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.

Bwana anakuja tuandae mioyo yetu;

Ujumbe wa Sefania ni unabii alioutoa wakati wa mfalme Yosia, mwana wa Amoni mfalme wa Yuda. Ni ujumbe wa hukumu iliyokuwa inaijia Yuda kama anavyotangulia kusema;

Sefania 1:2

[2]Nitavikomesha kabisa vitu vyote, visionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA.

Katika somo tulilopewa, tunaona Bwana akiahidi kuwaadhibu wakuu na watu wote wasiofuata sheria zake. Ni katika siku ile ya dhiki kuu ambayo Bwana atawaadhibu wote walioishi kinyume na neno lake. Mstari wa 17 unaeleza sababu ya ghadhabu ya Mungu kuwa ni kumtenda Bwana dhambi.

Ujumbe huu unatujia asubuhi hii, ukitukumbusha kuwa tukimtenda Bwana dhambi hatutaiepuka hukumu. Tufahamu kuwa kitakachotusaidia kuingia mbinguni, ni toba ya kweli, msamaha na Imani timilifu katika Kristo.

Bwana anakuja tuandae mioyo yetu.

Uwe na Alhamisi njema.

Amina.