Date: 
02-08-2017
Reading: 
Romans 6:15-23 NIV {Warumi 6:15-23]

WEDNESDAY  2ND AUGUST 2017 MORNING                

Romans 6:15-23  New International Version (NIV)

Slaves to Righteousness

15 What then? Shall we sin because we are not under the law but under grace? By no means! 16 Don’t you know that when you offer yourselves to someone as obedient slaves, you are slaves of the one you obey—whether you are slaves to sin, which leads to death, or to obedience, which leads to righteousness? 17 But thanks be to God that, though you used to be slaves to sin, you have come to obey from your heart the pattern of teaching that has now claimed your allegiance. 18 You have been set free from sin and have become slaves to righteousness.

19 I am using an example from everyday life because of your human limitations. Just as you used to offer yourselves as slaves to impurity and to ever-increasing wickedness, so now offer yourselves as slaves to righteousness leading to holiness. 20 When you were slaves to sin, you were free from the control of righteousness. 21 What benefit did you reap at that time from the things you are now ashamed of? Those things result in death! 22 But now that you have been set free from sin and have become slaves of God, the benefit you reap leads to holiness, and the result is eternal life. 23 For the wages of sin is death, but the gift of God is eternal life in[a] Christ Jesus our Lord.

Footnotes:

  1. Romans 6:23 Or through

The Apostle Paul wants us to understand that we are not saved by our good actions. We cannot do anything to earn our salvation. We are saved by Grace. It is a gift of God.

However this fact does not give us any excuse to continue sinning. We must do our best to repent and turn from sin. We should desire to please God by our words and actions and even by our pure thoughts. 

JUMATANO TAREHE  2 AGOSTI 2017 ASUBUHI                   

RUMI 6:15-23

15 Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha! 
16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki. 
17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; 
18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki. 
19 Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. 
20 Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. 
21 Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. 
22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. 
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu

 

Mtume Paulo anataka tuelewe kwamba hatuokolewi kwa sababu ya matendo yetu mema. Hatuwezi kufanya kitu kutupatanisha na Mungu. Ni kwa neema tu tunapokea zawadi ya wokovu kwa sababu Yesu ametufia msalabani. Pamoja na ukweli huu hatupaswi kucheza na dhambi. Tunapaswa kuchukia dhambi na kutubu na kuacha. Mungu atusaidieAC kuishi maisha yanayompendeza Mungu.