Date: 
12-07-2018
Reading: 
Romans 5:1-6 (Warumi 5:1-6)

THURSDAY 12TH JULY 2018  MORNING                                         

Romans 5:1-6 New International Version (NIV)

Peace and Hope

1 Therefore, since we have been justified through faith, we[a] have peace with God through our Lord Jesus Christ, through whom we have gained access by faith into this grace in which we now stand. And we[b]boast in the hope of the glory of God. Not only so, but we[c] also glory in our sufferings, because we know that suffering produces perseverance; perseverance, character; and character, hope. And hope does not put us to shame, because God’s love has been poured out into our hearts through the Holy Spirit, who has been given to us.

You see, at just the right time, when we were still powerless, Christ died for the ungodly.

Footnotes:

God loves each one of us. Because He loves us God sent His only son Jesus Christ to die for us so that our sins can be forgiven and we can be reconciled to God. Because of this all who repent and trust in Jesus have peace with God and we are no longer condemned.

Let us thank God for His Grace and love to us. Let us love and obey God and this will bring blessings to us and other people.   

 

ALHAMISI TAREHE 12 JULAI 2018  ASUBUHI                         

RUMI 5:1-6

1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, 
ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. 
Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; 
na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; 
na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. 
Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. 
 

Mungu anatupenda sisi sote. Kwa sababu Mungu anatupenda hataki tuangamie. Mungu alituma mwana wake wa pekee atufie msalabani ili dhambi zetu ziweze kusamehewa na tupatane tena na Mungu.  Kwa sababu  hii wote ambao wanatubu dhambi zao na kumwamini Yesu Kristo watasamehewa dhambi zao na kupatana na Mungu na hukumu haiku juu yao tena.

Tumshukuru Mungu kwa upendo wake na tumtii. Kufanya hivi italeta baraka kwetu na kwa watu wengine.