Date: 
18-08-2020
Reading: 
Romans 1:28-32

TUESDAY 18TH AUGUST 2020 MORNING                                                             ROMANS 1:28-32

Romans 1:28-32 New International Version (NIV)

28 Furthermore, just as they did not think it worthwhile to retain the knowledge of God, so God gave them over to a depraved mind, so that they do what ought not to be done. 29 They have become filled with every kind of wickedness, evil, greed and depravity. They are full of envy, murder, strife, deceit and malice. They are gossips, 30 slanderers, God-haters, insolent, arrogant and boastful; they invent ways of doing evil; they disobey their parents; 31 they have no understanding, no fidelity, no love, no mercy. 32 Although they know God’s righteous decree that those who do such things deserve death, they not only continue to do these very things but also approve of those who practice them.

 

Have you trusted in Jesus Christ to save you from God’s wrath?

We have to apply the gospel to our daily lives so that we overcome the sins that separate us from God.


JUMANNE TAREHE 18 AGOSTI 2020   ASUBUHI         

WARUMI 1:28-32

28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
30 wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.

Je, umemwamini Yesu Kristo ili akuokoe na hasira ya Mungu?

Tunahitaji kuishi sawa na mafundisho ya injili ili tuweze kushinda dhambi zinazotutenganisha na Mungu.