Date: 
28-08-2019
Reading: 
Revelations 22:10-15 (Ufunuo 22:10-15)

WEDNESDAY 28TH AUGUST 2019 MORNING                      

Revelation 22:10-15 New International Version (NIV)

10 Then he told me, “Do not seal up the words of the prophecy of this scroll, because the time is near. 11 Let the one who does wrong continue to do wrong; let the vile person continue to be vile; let the one who does right continue to do right; and let the holy person continue to be holy.”

Epilogue: Invitation and Warning

12 “Look, I am coming soon! My reward is with me, and I will give to each person according to what they have done. 13 I am the Alpha and the Omega, the First and the Last, the Beginning and the End.

14 “Blessed are those who wash their robes, that they may have the right to the tree of life and may go through the gates into the city. 15 Outside are the dogs, those who practice magic arts, the sexually immoral, the murderers, the idolaters and everyone who loves and practices falsehood.

 

Jesus will come back to earth in glory to judge the living and the dead. He will come at a time when no one expects Him. Let us be ready to welcome Him. Let us examine our lives and make sure we are trusting in Jesus Christ as your Lord and Savior. Also do your best to obey God’s commands and live to please Him. If we do this Jesus will welcome us into the joy of His presence in heaven. Let us not be left outside.


JUMATANO TAREHE 28 AGOSTI 2019 ASUBUHI   

UFUNUO 22:10-15

10 Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. 
11 Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. 
12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. 
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. 

Yesu Kristo atarudi tena duniani katika utukufu kuhukumu walio hai na wafu. Yesu atakuja wakati usiojulikana. Tujitahidi kuwa tayari kumlaki. Tuhakikishe tunamtegemea kama Bwana na Mwokozi wetu. Pia tujitahidi kutii amri zake na kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Kama tunafanya hivi Yesu atatukaribisha kuwa naye mbinguni. Tusiachwe nje.