Date: 
20-11-2019
Reading: 
Revelation 21:1-5 (Ufunuo 21:1-5)

WEDNESDAY 20TH NOVEMBER 2019  MORNING    

Revelation 21:1-5 New International Version (NIV)

A New Heaven and a New Earth

1Then I saw “a new heaven and a new earth,”[a] for the first heaven and the first earth had passed away, and there was no longer any sea. I saw the Holy City, the new Jerusalem, coming down out of heaven from God, prepared as a bride beautifully dressed for her husband. And I heard a loud voice from the throne saying, “Look! God’s dwelling place is now among the people, and he will dwell with them. They will be his people, and God himself will be with them and be their God. ‘He will wipe every tear from their eyes. There will be no more death’[b] or mourning or crying or pain, for the old order of things has passed away.”

He who was seated on the throne said, “I am making everything new!” Then he said, “Write this down, for these words are trustworthy and true.”

The Psalmist says, “As the deer pants for the water brooks, so my soul pants after you, God. (Psalm 42:1)

We long for life that is fulfilling and meaningful. We long to continue life, so God offers us eternal life. God satisfies needs that cannot be satisfied anywhere else.


JUMATANO TAREHE 20 NOVEMBA 2019  ASUBUHI                                     

UFUNUO 21:1-5

1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.

Mwandishi wa Zaburi anasema, “kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji, Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. (Zaburi 42:1)

Tuna shauku na maisha yenye maana na utimilifu. Tuna shauku ya kuendelea kuishi, hivyo Mungu anatupa uzima wa milele. Mungu hutosheleza mahitaji yale ambayo hakuna mwingine anayeweza kufanya hivyo popote.