Date: 
14-05-2020
Reading: 
Psalm 98:1-4 (Zaburi 98:1-4)

THURSDAY 14TH MAY 2020    MORNING   PSALM 98:1-4

Psalm 98:1-4  New International Version (NIV)

1 Sing to the Lord a new song,
    for he has done marvelous things;
his right hand and his holy arm
    have worked salvation for him.
The Lord has made his salvation known
    and revealed his righteousness to the nations.
He has remembered his love
    and his faithfulness to Israel;
all the ends of the earth have seen
    the salvation of our God.

Shout for joy to the Lord, all the earth,
    burst into jubilant song with music;

 

Many of the psalms were written during personal distresses experienced by God’s people.

When we see all that is happening in the world, and as we consider our own personal struggles in life, how can we find joy and hope? We know that God will act on behalf of his people.

It is by his own power that he brings victory for himself. This is the great hope we have; God will act for his own purposes and to defend his own name and holiness. 


ALHAMISI TAREHE 14 MEI 2020    ASUBUHI                                                     

ZABURI 98:1-4

1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu.
Mshangilieni Bwana, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.

Zaburi nyingi ziliandikwa katika nyakati ambazo watu wa Mungu walipita katika vipindi vigumu.

Tunapoyaona haya yote yanayotokea katika dunia hii, na tunapofikiri kuhusu mahangaiko tunayopitia katika maisha, tunajiuliza; tutapata wapi furaha na matumaini? Tunajua kuwa Mungu atasimama kwa ajili ya watu wake.

 Ni kwa nguvu zake mwenyewe, Mungu atajitwalia ushindi. Hili ndilo tumaini kuu tulilo nalo; ya kwamba Mungu atatenda ili atimize kusudi lake na kulitetea Jina lake na utakatifu wake.