Date: 
22-07-2019
Reading: 
Philippians 4:8-9

MONDAY 22ND JULY 2019 MORNING                                     

Philippians 4:8-9 New International Version (NIV)

Finally, brothers and sisters, whatever is true, whatever is noble, whatever is right, whatever is pure, whatever is lovely, whatever is admirable—if anything is excellent or praiseworthy—think about such things. Whatever you have learned or received or heard from me, or seen in me—put it into practice. And the God of peace will be with you.

This week we are thinking about Christian Discipleship.  The Apostle Paul advises the Christians in Philippi that their thoughts are important. This is also true for us. Whatever we say or do begins in our thoughts. We must fill our minds with good thoughts so that we will live to please God.  Meditating daily on the Word of God in the Bible is a very important part of this.


JUMATATU TAREHE 22 JULAI 2019 ASUBUHI                              

WAFILIPI 4:8-9     

Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. 
Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi. 

Wiki hii tunatafakari kuhusu Ufuasi na Uanafunzi.  Mtume Paulo anashauri Wakristo kule Filipi kuhusu mawazo yao.  Mawazo yetu ni muhimu. Kila kitu tunachosema au tunachoyofanya kinaanzia katika mawazo yetu. Tunapaswa kufikiri mambo mema ili tuwezi kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Kusoma na kutafakari Neno la Mungu katika Biblia kila siku ni muhimu sana.