DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKAn TAREHE 26 APRILI, 2026
SIKU YA BWANA YA 3 BAADA YA PASAKA
MPIGIENI BWANA KELELE ZA SHANGWE. NENO LINALOTUONGOZA NI:
“NDANI YA KRISTO TUNAKUWA WAPYA”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. MATOLEO YA TAREHE 19/04/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 19/04/2026 ni Washarika 885
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Jumapili ijayo tarehe 03/05/2026 tutamtolea Mungu fungu la Kumi. Washarika tujiandae. Aidha siku hiyo itakuwa ni Kantate Domino – Mwimbieni Bwana Wimbo mpya. Makabila yatakayokuwa tayari kuimba wajiandikishe ofisi ya Mchungaji.
8. Uongozi wa Kwaya ya Umoja unapenda kuwatangazia Wanakwaya wa vikundi vyote vya usharika kuwa Jumanne ijayo tarehe 28/04/2026 saa 11.00 jioni kutakuwa na mazoezi ya uimbaji kwa ajili ya maandalizi ya Kantate. Wanakwaya wote mnaombwa kuhudhuria na kufika kwa wakati.
9. Leo tarehe 26/04/2026 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika karibuni.
10. Baba Askofu, Dkt, Alex Gehaz Malasusa anawaalika wazee wote wa Baraza kushiriki ibada ya shukrani itakayofanyika katika Usharika wa Mbezi Beach siku ya Jumamosi tarehe 02/05/2026 kuanzia saa 3.00 asubuhi. Ibada hiyo itaongozwa na Baba Askofu mwenyewe.
11. Uongozi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani unapenda kuwataarifu kuwa kutakuwa na semina juu ya uendeshaji wa harambee na changizo kwa ajili ya miradi na maendeleo ya Kanisa katika ngazi mbalimbali. Semina hiyo imeandaliwa na kuratibiwa na Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (DarTU) kwa ushirikiano wa United Evangelical Mission (UEM). Semina itafanyika kesho jumatatu tarehe 27/04/2026 kuanzia saa 3.30 asubuhi hadi saa 7.30 mchana katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha DarTU Mwenge. Mnenaji Mkuu anatarajiwa kuwa Prof. Dr. Michael Vilain kutoka Ujerumani.
12. Alhamisi ijayo tarehe 30/04/2026 Kwaya Kuu ya Usharika itakuwa na safari ya kwenda Morogoro mpaka tarehe 03/05/2026 kwa lengo la kufanya Mkutano Mkuu wa Kwaya. Washarika tuiombee safari hiyo na Mkutano huo. Mungu awabariki sana
13. Familia ya Bwana na Bibi Jimmy Whitsun Moshi wamepata zawadi ya mtoto wa kike mwezi Machi. Mama, Baba na mtoto wanaendelea vizuri.
14. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 03/05/2026 katika ibada ya tatu
- Familia ya Bwana na Bibi Sebastian Kolowa watamshukuru Mungu kwa ukuu wake katika maisha ya familia yao.
Neno: Zaburi 40:5, Wimbo: TMW 255
15. NDOA. NDOA WASHARIKA
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 09/05/2026
SAA 9.00 ALASIRI
-
Bw. Fredrick Leonard Kowero na Bi. Anitha Frank Saria.
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
16. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mamkwe
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Francis Mwaitembo
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Itemba
- Oysterbay na Masaki: Kwa Dr Malentlema
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Askofu na Mama Alex Malasusa.
- Upanga: Kwa Mama Violet Maro.
17. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
18. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
