Date: 
17-12-2025
Reading: 
Mathayo 3:1-4

Jumatano asubuhi tarehe 17.12.2025

Mathayo 3:1-4

1 Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,

2 Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

3 Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.

4 Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.

Itengenezeni njia ya Bwana;

Leo tunamsoma Yohana Mbatizaji kwenye Injili ya Mathayo. Mathayo anamrejea Yohana akihubiri katika nyika ya Uyahudi na kusema tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Yohana aliendelea kuwaambia watu waitengeneze njia ya Bwana na kuyanyoosha mapito yake. 

Yohana alikuwa anatimiza utabiri wa Nabii Isaya kama tulivyoona na kusikia katika mahubiri ya Jumapili iliyopita, kama mtangulizi aliyeleta habari za ujio wa Yesu Kristo. Kwa utimilifu huo Yesu alikuja, Yesu yupo, na atarudi tena kuwahukumu walio hai na wafu. Tengeneza maisha yako uwe na mwisho mwema. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com