DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 09 NOVEMBA, 2025
SIKU YA BWANA YA 3 KABLA YA MAJILIO
NENO LINALOTUONGOZA NI
TUVUMILIE HATA MWISHO KATIKA BWANA
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 26/10/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 26/11/2025 ni Washarika 557 Sunday School …..
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Leo tarehe 09/11/2025 tutamtole Mungu fungu la kumi. Washarika Karibuni.
8. Uongozi wa umoja wa vijana idara ya Michezo unapenda kuwakaribisha washarika wote kwenye mazoezi ya maandalizi ya igizo la Christmas, mazoezi hayo yataanza mapema jumatatu tarehe 10/11/2025, yatafanyika kila siku ya jumatatu saa 11.00 jioni na jumamosi saa 10.00 jioni kwenye ukumbi wetu wa chini. karibuni wote kutumika shambani mwa Bwana.
9. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia kuwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa kipaimara kwa mwaka wa Kwanza na wa pili yatafanyika tarehe 22/11/2025 kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 8.00 mchana hapa usharikani. Wale waliopata kipaimara kuanzia miaka 3 iliyopita wanakaribishwa kwenye mafundisho haya.
10. Tarehe ya ubarikio kwa watoto wa Kipaimara kwa Kiswahili itakuwa ni tarehe 29/11/2025 na kwa Kingereza itakuwa ni tarehe 06/12/2025. Mavazi kwa wavulana ni Suti nyeusi au suruali nyeusi na shati nyeupe ya mikono mirefu viatu vyeusi. Wasichana gauni jeupe la heshima na viatu vyeupe.
11. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA
KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 15/11/2025
SAA 9.00 ALASIRI
-
Bw. Leslie Mwesiga Lwezaula na Bi. Eliwandisha Gerson Lyanga
KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 22/11/2025 AMBAYO ITAFUNGWA KANISA KUU LA ST. JOSEPH POSTA KATI YA
-
Bw. Arnord Bernald na Bi. Merian Kaleb Kabezi
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
- Upanga: Kwa Mama Magembe
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Moses Kombe
- Mjini kati: Itafanyika jumamosi hapa kanisani saa 1.00 asubuhi
- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
14. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
