Date: 
21-08-2025
Reading: 
1 Wafalme 3:28

Alhamisi asubuhi tarehe 21.05.2025

1 Wafalme 3:28

Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.

Tuenende kwa hekima ya Mungu;

Mfalme Suleimani alitokewa na Mungu akaambiwa aombe atakalo, akaomba hekima ili aweze kutawala kwa haki. Basi siku moja wakaja wanawake wawili makahaba wakigombea mtoto. Hawa kila mmoja alikuwa na mtoto, ila mmoja akamlalia mtoto wake usiku akafa, na alipoona amekufa akambadilisha na mtoto wa mwenzake. Wakaenda kuamuliwa mbele ya Mfalme. Mfalme akaamuru mtoto aliye hai akatwe wagawiwe, yule ambaye ni mama yake alimwonea huruma mwanae, akasema asikatwe, yule ambaye mtoto siyo wake akasema akatwe! Mfalme akaamuru yule wa kwanza apewe mtoto.

Ndipo linakuja somo la leo asubuhi, kwamba Israeli wote walipata habari za hukumu ile aliyoitoa Mfalme, nao wakamuogopa sana maana waliona kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake. Bila shaka Mfalme Suleimani alipata kuamua kwa haki kwa sababu alikuwa na hekima aliyoomba kwa Mungu akapewa. Nini itikio letu? Tukiwa na Yesu tunatenda kwa Utukufu wake maana tunatenda kwa hekima itokayo kwake. Amina

Alhamisi njema

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com