Date: 
20-08-2025
Reading: 
Luka 7:31-35

Jumatano asubuhi tarehe 20.05.2025

Luka 7:31-35

31 Bwana akasema, Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Nao wamefanana na nini?

32 Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema, Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.

33 Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo.

34 Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.

35 Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.

Tuenende kwa hekima ya Mungu;

Yesu alikuwa anafundisha juu ya habari za Yohana Mbatizaji, baadhi ya watu na watoza ushuru wakaamini na kukiri kwamba walibatizwa kwa ubatizo wa Yohana. Lakini Mafarisayo walikataa kubatizwa kwa huo ubatizo wa Yohana. Ndipo katika somo Yesu anaanza kwa kusema "niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki?" Yesu aliona hawana uelekeo maana hawakuamini alichokifundisha.

Kutokuamini ujio na ujumbe wa Yohana Mbatizaji ilikuwa kutomwamini Yesu, maana Yohana alitangaza ujio wa Yesu Kristo. Yohana aliwaita watu kutubu na kubatizwa, tayari kumpokea Yesu Kristo. Kutoamini ujumbe wa Yesu haikuwa hekima kwa mujibu wa mstari wa 35. Hekima ya kweli ni kumwamini Yesu Kristo aliye njia ya kweli na uzima. Amina

Jumatano njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com