Date: 
30-12-2024
Reading: 
Isaya 25:9

Hii ni Noeli

Jumatatu asubuhi tarehe 30.12.2024

Isaya 25:9

[9]Katika siku hiyo watasema, 

Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, 

Ndiye tuliyemngoja atusaidie; 

Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, 

Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.

Waliomngojea Mwokozi wamuona;

Tunausoma wimbo ambao Nabii Isaya anasema utaimbwa na Taifa la Mungu lililokombolewa toka kwenye udhalimu. Hii ni baada ya Bwana aliyengojewa kuwaokoa watu wake.

Katika majira haya, nasi tunapoendelea kuimba wimbo wa sifa na Utukufu katikati ya kumbukumbu ya Yesu Kristo kuzaliwa kwa ajili ya wokovu wetu, sifa na shukrani zetu ziendane na matendo mema katika kuutangaza Ufalme wake, ili ulimwengu wote uokolewe katika yeye. Amina

Jumatatu njema

Heri Buberwa