Date: 
21-12-2024
Reading: 
Zekaria 8:9-15

Hii ni Advent 

Jumamosi asubuhi tarehe 21.12.2024

Zekaria 8:9-15

9 Bwana wa majeshi asema hivi, Mikono yenu na iwe hodari, ninyi mnaosikia siku hizi maneno haya kwa vinywa vya manabii, waliokuwapo siku hiyo ulipowekwa msingi wa nyumba ya Bwana wa majeshi; yaani, hekalu hilo; ili lijengwe.

10 Maana kabla ya siku zile hapakuwa na ijara kwa mwanadamu, wala hapakuwa na ijara kwa mnyama; wala hapakuwa na amani kwake yeye aliyetoka, wala kwake yeye aliyeingia, kwa sababu ya adui; nami nalimwacha kila mtu kugombana na jirani yake.

11 Lakini sasa sitakuwa kwa mabaki ya watu hawa kama nilivyokuwa siku zile za kwanza, asema Bwana wa majeshi.

12 Kwa maana itakuwako mbegu ya amani; mzabibu utatoa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na hizo mbingu zitatoa umande wake; nami nitawarithisha mabaki ya watu hawa vitu hivi vyote.

13 Kisha itakuwa, kama vile mlivyokuwa laana katika mataifa, Ee nyumba ya Yuda, na nyumba ya Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka; msiogope, lakini mikono yenu na iwe hodari.

14 Maana Bwana wa majeshi asema hivi, Kama vile nilivyoazimia kuwatenda ninyi mabaya, baba zenu waliponikasirisha, asema Bwana wa majeshi, wala mimi sikujuta;

15 vivyo hivyo nimeazimia katika siku hizi kuutendea Yerusalemu mema, na nyumba ya Yuda pia; msiogope.

Tubuni na kuiamini Injili;

Bwana anamtuma Zekaria kutangazia watu wake kusikia maneno ya manabii waliotumwa, kuutangaza ufalme wake. Na kwa njia hiyo anaahidi kuitendea Yerusalemu mema.

Sauti ya Bwana inatujia ikitutaka kuitengeneza njia yake. Ni baraka kwetu tukisikia na kutii sauti yake, na Mungu anaahidi mema kwetu tukifanya hivyo. Umeitengeneza njia ya Bwana? Umetubu na kuiamini Injili? Wakati ni sasa, mwamini Yesu uokolewe.

Jumamosi njema 

Heri Buberwa