Date: 
17-12-2024
Reading: 
Eziekiel 3:16-19

Hii ni Advent 

Jumanne asubuhi tarehe 17.12.2024

Ezekieli 3:16-19

16 Hata ikawa, mwisho wa siku saba, neno la Bwana likanijia, kusema,

17 Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu.

18 Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

Tubuni na kuiamini Injili;

Ezekieli anatumwa kupeleka ujumbe wa Bwana kwa watu wake, kwamba watu wazingatie maonyo ya Bwana. Ezekieli anatumwa awaambie watu kuwa wapatapo ujumbe wa Bwana waupokee na kuufanyia kazi. Wakipokea maonyo ya Bwana wayazingatie, kinyume chake watakufa katika uovu.

Ujumbe wa somo hili asubuhi hii ni kumsikiliza Mungu anavyosema nasi katika maisha yetu. Tunamsikiliza Mungu tunapomwamini na kulishika neno lake, ambao ndiyo mwongozo pekee usiokosea. Kwa njia ya neno la Mungu tunatubu na kuiamini Injili kuelekea uzima wa milele. Amina

Jumanne njema 

Heri Buberwa