Date: 
16-12-2024
Reading: 
Isaya 19:19-22

Hii ni Advent 

Jumatatu asubuhi tarehe 16.12.2024

Isaya 19:19-22

[19]Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa BWANA, na nguzo mpakani mwake kwa BWANA.

[20]Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa.

[21]Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza.

[22]Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya.

Tubuni na kuiamini Injili;

Bwana anatangaza baraka kwa watu wake, ambapo anatangaza kuwabariki wote watakaomlilia. Mungu anaonesha huruma yake kwa wamwitao, akiwasamehe na kuwabariki.

Bwana anatangaza baraka kwetu asubuhi hii. Pale tutakapomuita atakuja, atatusamehe dhambi zetu na kutuponya, akituingiza katika uzima wa milele. Tutubu na kuiamini Injili. Amina

Uwe na wiki njema

 

Heri Buberwa