Date: 
13-12-2024
Reading: 
Isaya 46:8-13

Hii ni Advent 

Ijumaa asubuhi tarehe 13.12.2024

Isaya 46:8-13

[8]Kumbukeni haya, mkajionyeshe kuwa waume; jifahamisheni haya, ninyi mkosao;

[9]kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;

[10]nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.

[11]Nikiita ndege mkali kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyo mbali; naam, nimenena, nami nitatekeleza; nimekusudia, nami nitafanya.

[12]Nisikilizeni, ninyi mlio na moyo mshupavu, mlio mbali na haki;

[13]Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.

Ukombozi wetu umekaribia;

BWANA anamtuma Isaya kuleta ujumbe, kwamba yeye ndiye Mungu, na hakuna mwingine kama yeye. Anauita ulimwengu wote kumtii yeye.

Ni tangazo la ufalme, kuwa Yesu Kristo alikuwepo, yupo na atakauwepo. Hivyo tumkiri na kumfuata kwa uaminifu, ili ajapo kulichukua Kanisa tuurithi uzima wa milele. Amina

Ijumaa njema

 

Heri Buberwa 

Mlutheri