MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 23 JUNI, 2024

SIKU YA BWANA YA 4 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI

IWENI NA HURUMA 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. ili tuwakaribishe.

3. Matoleo ya Tarehe 16/06/2024

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

5. Kitenge chetu cha kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya shilingi 40,000/= 

6. Uongozi wa Umoja wa vijana unapenda kuwatangazia vijana wote mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu ya vijana. Mazoezi yatafanyika siku ya ijumaa saa 11.30 jioni na Jumamosi saa 8.00 mchana. Vijana wote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kwa wakati.

8. Alhamisi ijayo tarehe 27/06/2024 na Ijumaa 28/06/2024 kutakuwa na kambi ya watoto hapa kanisani kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni. Tafadhali tuwalete watoto ili waweze kufundishwa mambo ya afya, imani na mambo mengi kutoka kwa wanenaji. Tunawakaribisha watoto wote wa Sunday school na walioko mafundisho, pia wale waliopata kipaimara mwaka jana wanakaribishwa.

9. SHUKRANI. JUMAPILI IJAYO TAREHE 30/06/2024 KATIKA IBADA YA KWANZA SAA 1.00 ASUBUHI

  • Familia ya Andrew Kuzilwa watamshukuru Mungu kwa kumponya Mama kwenye ajali mbaya ya gari, Ulinzi na afya njema kwa familia, kumponya mke wake Alfredina Kuzilwa pamoja na mambo meng aliyowatendea.

Neno: Zab. 116:1-8, Wimbo: TMW 295

 IBADA YA PILI SAA 4.30 ASUBUHI

  • Nengai na Esuvat Mollel, watamtolea Mungu sadaka ya Shukrani kwa Baraka na Ulinzi wake na kufika umri wa miaka 50 tarehe 30/06/2024 Pamoja na mambo mengi aliyowatendea.

 10. NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 16/07/2024 SAA 9.00 ALASIRI KATI YA

  • Bw. Innocent Michael Temba na Bi. Esther John Msuya

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: kwa ………………………………………
  • Mjini kati: Watafanya ibada hapa Usharikani.
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo:Kwa Bwana na Bibi Mtunga
  • Kinondoni: Kwa …………………………….
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Frank Mwaitembo
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Eng. na Bibi Harold Temu
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa ………….
  • Oysterbay, Masaki: Kwa ………………………

13. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza

Na huu ndiyo mwisho wa mata

ngazo yetu, Bwana ayabariki.