Date: 
23-05-2024
Reading: 
Waefeso 1:13-14

Alhamisi asubuhi tarehe 23.05.2024

Waefeso 1:13-14

13 Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.

14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.

Roho Mtakatifu kwa kila aaminiye;

Mtume Paulo anaanza waraka wake kwa waefeso kwa kumshukuru Mungu aliyewaokoa wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo. Kristo huyu ndiye neno aliyeleta wokovu kama tunavyosoma katika mstari wa 13. Anawasihi Waefeso kudumu katika Kristo huyo ambaye aliwaacha na ahadi ya Roho Mtakatifu alipopaa. 

Tunapomsoma Paulo akiwakumbusha waefeso kuhusu ahadi ya Roho Mtakatifu, tunakumbushwa nasi kuwa ahadi hii ipo kwetu, kwamba tunaye Roho Mtakatifu tuliyempokea tulipoamini. Hii ni kwa sababu tunapomwamini Yesu Kristo tunampokea Roho Mtakatifu mioyoni mwetu. Kristo anatosha. Amina.

Alhamisi njema

 

Heri Buberwa