Date: 
21-05-2024
Reading: 
Yohana 14:26-18

Hii ni Pentekoste 

Jumanne asubuhi tarehe 21.05.2024

Yohana 14:16-18

16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;

17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.

18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

Roho Mtakatifu kwa kila aaminiye;

Yesu alikuwa akiwaambia wanafunzi wake kuhusu yale ambayo yangempata. Aliwaambia kuhusu kufa, kufufuka na kuondoka kwake. Ndipo anapowapa ahadi ya kutowaacha yatima, bali kuwaachia msaidizi aliye Roho Mtakatifu. Alijua angewaambia moja kwa moja kwamba angeondoka labda wangeogopa na kukosa tumaini. Lakini anawapa ahadi ya Roho Mtakatifu ili wabaki na tumaini katika yeye.

Ni kweli baada ya Yesu kufufuka alipaa mbinguni, na baada ya siku hamsini aliwashushia Roho Mtakatifu Mitume wake siku ile ya Pentekoste. Roho Mtakatifu huyu ndiye tuliyempokea tulipomkiri na kumwamini Yesu Kristo. Kumbe ahadi ya Roho Mtakatifu hudumu kwetu hata sasa. Basi tuombe neema ya Mungu, tuzidi kuongozwa na Roho Mtakatifu katika safari yetu ya imani ili tuwe na mwisho mwema. Amina.

Jumanne njema 

 

Heri Buberwa