Date: 
17-05-2024
Reading: 
1 Timotheo 2:1-3

Ijumaa asubuhi tarehe 17.05.2024

1 Timotheo 2:1-3

1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.

3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;

Omba! Mungu anasikia kuomba kwetu;

Mtume Paulo anamuelekeza Timotheo kwamba sala zifanyike kwa ajili ya watu wote. Paulo anaelekeza sala kufanyika kwa ajili ya watu wote, kuanzia watu mmoja mmoja hadi kwa viongozi. Paulo anasema sala huleta maisha ya utulivu, maana Bwana hujibu sala za wamuombao.

Anachokisema Paulo ni kundi la waaminio kuwa na maisha ya ibada, maisha ambayo ni ya kumtegemea Bwana. Hapa naweza kusema kuwa Paulo anatukumbusha kumwabudu na kumuomba Yesu Kristo aliye Bwana wa Kanisa. Ni kwa njia ya sala Kristo hutupa haja zetu, maana yeye husikia kuomba kwetu. Kwa hiyo tuombe, maana Bwana husikia kuomba kweru. Amina.

Ijumaa njema

 

Heri Buberwa