Date: 
28-12-2023
Reading: 
Tito 2:11-14

Alhamisi asubuhi tarehe 28.12.2023

Tito 2:11-14

11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;

12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;

13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;

14 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.

Tunaitwa kuwa Mashahidi wa Kristo;

Mtume Paulo anamuelekeza Tito kufundisha juu ya mwenendo wa waaminio. Sura ya pili inaelekeza juu ya mwenendo wa wazee, vijana, watumwa, na kila mtu kwa nafasi yake. Wazee wanaitwa kuwa wenye kiasi na utakatifu, vijana kuwa na kiasi, watumwa kuwatii Bwana zao n.k

Sasa katika somo la asubuhi ya leo, Mtume Paulo anamuelekeza Tito awafundishe watu kuwa na mwenendo ufaao, akisema kuwa neema ya Mungu iokoayo imefunuliwa. Neema hii huwafundisha watu kukataa ubaya na tamaa za dunia, ili waishi wakimshuhudia Kristo. Yesu ndiye mwenye neema hii iokoayo, ituwezeshayo kukataa ubaya na kushika mwenendo mwema. Mwamini sasa uokolewe. Amina.

 

Heri Buberwa