Date: 
21-12-2023
Reading: 
Zekaria 3:1-17

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 21.12.2023

Zekaria 3:1-7

1 Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.

2 Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?

3 Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.

4 Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi.

5 Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa Bwana akasimama karibu.

6 Kisha malaika wa Bwana akamshuhudia Yoshua, akisema,

7 Bwana wa majeshi asema hivi, Kama ukienda katika njia zangu, na kama ukishika maagizo yangu, ndipo utakapoihukumu nyumba yangu, nawe utazilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.

Itengenezeni njia ya Bwana;

Zekaria alioneshwa Yoshua Kuhani Mkuu akiwa amesimama mbele ya malaika, shetani akiwa amesimama mkono wake wa kuume kushindana naye. Bwana alimkemea shetani! Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu, mara akavalishwa nguo safi. Yoshua anashuhudiwa kwenda katika njia Mungu, ili apewe nafasi ya kumkaribia Mungu.

Yoshua anaonekana kusimama kwa kazi ya Bwana kwa nguvu yake Bwana aliyemuita. 

Nguvu hii aliyopewa Yoshua kuifanya kazi ya Mungu, sisi tunaipata kwa njia ya Yesu Kristo. Yesu Kristo akikaa kwetu tunakuwa na nguvu ya kumtumikia, na maisha yetu yote yanakuwa ni ya kumuishia yeye. Tudumu katika Kristo tukijiandaa kumpokea. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa