Date: 
11-12-2023
Reading: 
Isaya 11:10

Hii ni Advent;

Jumatatu asubuhi tarehe 11.12.2023

Isaya 11:10

Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu.

Yesu anakuja katika Utukufu wake;

Isaya anaianza sura ya 11 kwa kutabiri ujio wa Kristo Yesu. Anasema Mfalme atazaliwa kutokea kwenye uzao wa Yese;

Isaya 11:1-2

1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.
2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;

Huu ni unabii unaotabiri kuzaliwa kwa Yesu Kristo, kama Mwokozi wa ulimwengu.

Sasa katika mstari wa 10, tunasoma shina la Yese (Kristo) kutafutwa na watu, na mahali pake pa kupumzikia patakuwa pa Utukufu.

Hapa anatajwa Yesu Kristo ambaye atakuja kwa ajili ya ukombozi wa watu wote, na atarudi kwa Utukufu kulichukua Kanisa. 

Tujiandae kumpokea. Amina

Uwe na wiki njema

 

Heri Buberwa