Date: 
16-11-2023
Reading: 
Luka 21:14-19

Alhamisi asubuhi tarehe 16.11.2023

Luka 21:14-19

14 Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu;

15 kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.

16 Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu.

17 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.

18 Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu.

19 Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.

Mwenye kuvumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka;

Yesu alikuwa akifundisha juu ya siku za mwisho, akielezea mambo ambayo yangetokea;

Luka 21:10-11

10 Kisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme;
11 kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.

Sasa katikati ya yote hayo anawatuma kuifanya kazi yake akiwatia moyo kama somo linavyosomeka. Anawaambia kuvumilia usaliti wa ndugu na chuki. 

Katika mstari wa 19 Yesu anawaambia kuwa kwa subira wataziponya nafsi zao. Subira hii ndiyo tunakumbushwa kuwa nayo asubuhi hii, kwamba tuvumilie katika Bwana hata mwisho ili tuuone ufalme wake. Mshike Kristo siku zote za maisha yako bila kumuacha kamwe hata mwisho, ili arudipo asikuache. Amina.

Alhamisi njema 

Heri Buberwa