Date: 
11-11-2023
Reading: 
Luka 6:20-22

Jumamosi asubuhi tarehe 11.11.2023

Luka 6:20-22

20 Akainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, Heri ninyi mlio maskini, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu.

21 Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka.

22 Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.

Uenyeji wa mbinguni;

Katika sehemu hii Luka anaandika kwa ufupi hotuba ya mlimani (Luka 6:20-22) akiifupisha ukifananisha kama ilivyoandikwa katika Injili ya Mathayo sura ya 5 hadi 7. Luka anaandika kwa ufupi, Yesu akifundisha waaminio walivyotakiwa kuishi katika njia ya ufuasi.

Mistari tuliyosoma inaongelea heri wenye njaa maana watashibishwa, walio maskini ufalme wa Mungu ni wao, na wamtumainio Bwana kuurithi uzima wa milele. Wito kwetu ni kudumu katika imani hii, ili siku moja tuingie uzimani. Amina.

Siku njema.

 

Heri Buberwa 

Mlutheri