Date: 
20-10-2023
Reading: 
Luka 8:49-56

Ijumaa asubuhi tarehe 20.10.2023

Luka 8:49-56

49 Alipokuwa akinena hayo, alikuja mtu kutoka nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akamwambia, Binti yako amekwisha kufa; usimsumbue mwalimu.

50 Lakini Yesu aliposikia hayo, alimjibu, Usiwe na hofu, amini tu, naye ataponywa.

51 Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.

52 Na watu wote walikuwa wakilia na kumwombolezea; akasema, Msilie, hakufa huyu, bali amelala usingizi tu.

53 Wakamcheka sana, maana walijua ya kuwa amekwisha kufa.

54 Akamshika mkono, akapaza sauti, akisema Kijana, inuka.

55 Roho yake ikamrejea, naye mara hiyo akasimama. Akaamuru apewe chakula.

56 Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini akawakataza wasimwambie mtu lililotukia.

Imani isiyo na mashaka;

Yairo alikuwa amemfuata Yesu kuomba amponye mtoto wake aliyekuwa mgonjwa. Ukisoma nyuma kidogo unaona hapa;

Luka 8:41-42

41 Na tazama, mtu mmoja akaja, jina lake Yairo, naye ni mtu mkuu wa sinagogi, akaanguka miguuni pa Yesu, akamsihi aingie nyumbani kwake;
42 kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.

Sasa somo tulilosoma ni jinsi Yesu alivyokwenda nyumbani kwa Yairo kumponya mtoto wake. Kubwa linaloonekana hapa ni imani aliyokuwa nayo Yairo, akamwendea Yesu kuomba uponyaji wa mwanae. Bila shaka alikuwa na imani isiyokuwa na mashaka, kwamba Yesu angemponya mtoto wake. Nasi tunaalikwa kuwa na imani isiyo na mashaka katika Kristo. Amina.

Ijumaa njema.

Heri Buberwa