Date: 
14-10-2023
Reading: 
Warumi 9:25-33

Jumamosi asubuhi tarehe 13.10.2023

Warumi 9:25-33

25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.

26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.

27 Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa Israeli,ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari,ni mabaki yao tu watakaookolewa.

28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.

29 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora.

30 Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani;

31 bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria.

32 Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo,

33 kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika.

Uhuru wa Mkristo;

Mtume Paulo anawarejea manabii Hosea na Isaya, kwa ahadi ya Mungu kulitunza Taifa lake. Mungu aliahidi kuwatunza watu wake, akawapa sheria ili waishi kwa kumfuata. Hosea anatumia lugha ya "Bwana kuwaita watu wake..." Isaya yeye anaonya juu wa wasiofuata sheria kuangamia. Wote wanaonesha lengo la Mungu kuwatunza na kuwaokoa watu wake, kwa kutii sheria zake.

Mtume Paulo kwenye mstari wa 33 anamalizia kwa kusema kuwa kila aaminiye hatatahayarika. Paulo anaweka msingi wa uhuru kwa kuokolewa na Kristo kwa njia ya imani katika njia ya ufuasi. Kwamba tunaokolewa kwa neema, kwa njia ya imani. Hatuishi kwa sheria tena, bali kwa neema ya Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Mwamini sasa uokolewe. Amina.

Jumamosi njema 

Heri B