Date: 
06-10-2023
Reading: 
Mithali 4:10-11

Ijumaa asubuhi tarehe 06.10.2023

Mithali 4:10-11

10 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.

11 Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.

Tuwalee watoto katika njia ya Bwana;

Mithali tunayosoma leo asubuhi ni juu ya kulishika neno la Mungu. Mwandishi anatumia maneno "kuzipokea kauli zangu" ili miaka ya maisha kuwa mingi. Mwandishi anaelekeza kuwa kulishika neno la Mungu ndiyo msingi wa maisha ya mwanadamu. Katika neno la Mungu ipo hekima ituongozayo katika njia ya ufuasi. 

Mwandishi anatukumbusha kulishika neno la Mungu kama Yesu alivyosema;

Yohana 8:51

Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.

Wito wangu kwako asubuhi hii ni sisi sote kulishika neno la Mungu ili tuwe na mwisho mwema. Amina.

Ijumaa njema.

 

Heri Buberwa