Date: 
12-06-2023
Reading: 
Mathayo 16:21-26

Jumatatu asubuhi tarehe 12.06.2023

Mathayo 16:21-27

21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.

22 Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.

23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.

24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.

26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?

27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

Mungu au Ulimwengu;

Yesu anatoa taarifa ya yeye kuiendea njia ya mateso, kufa na kufufuka kwa ajili ya ulimwengu. Petro yeye hakukubali, akakataa akamkemea Yesu!!? Eti ni uongo hayo hayatampata! Yesu akamkemea kwa maneno yake hayo.

Sasa baada ya kuwapa ujumbe huo, ndipo Yesu anawaambia wanafunzi kwamba yeyote atakaye kumfuata ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake amfuate (Yesu). Yesu anakazia kuwa haifai mtu kupata mambo ya dunia hii halafu akaukosa uzima wa milele. Yesu anasisitiza kila mtu kulipwa kadri ya matendo yake pale atakaporudi tena.

Ujumbe wa Yesu kwa wanafunzi ulihusu kumfuata yeye. Ujumbe uliwaambia kumchagua Yesu au Ulimwengu, ndiyo maana aliwaambia kujikana na kumfuata yeye. Sisi nasi asubuhi hii tunaalikwa kujikana wenyewe na kumfuata Yesu. Tuchague kumfuata Mungu, na siyo Ulimwengu.

Uwe na wiki njema 

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com