Date: 
10-06-2023
Reading: 
Kutoka 3:11-14

Jumamosi asubuhi tarehe 10.06.2023

Kutoka 3:11-14

11 Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri?

12 Akasema, Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.

13 Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini?

14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.

Mungu mmoja; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;

Musa alipotumwa na Mungu kwenda kwa Farao kupeleka ujumbe wa Israeli kuondoka Misri, aliogopa akijiuliza ataendaje. Mungu akamwambia atakuwa pamoja naye. Musa akauliza tena awaambie Israeli nani kanituma kuwachukua? Tunasoma Mungu akimjibu waambie ni MIMI NIKO AMBAYE NIKO, ndiye amenituma kwenu.

Mungu tangu mwanzo alipanga kuwakomboa watu wake. Tulichokisoma ulikuwa mpango wa Mungu kuwakomboa Israeli toka utumwani Misri. Mpango haukuishia hapo, Mungu Baba alimtuma mwana wake Yesu Kristo akatuokoa kwa njia ya kifo msalabani. Baada ya kupaa, Yesu akatuachia Roho Mtakatifu. Katika Utatu Mtakatifu tumesamehewa dhambi zetu na kuokolewa. Tudumu katika imani katika Mungu wa Utatu Mtakatifu. Amina.

Uwe na Jumamosi tulivu

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650