Date: 
02-06-2023
Reading: 
Matendo ya Mitume 13:6-12

Hii ni Pentekoste 

Ijumaa asubuhi tarehe 02.06.2023

Matendo ya Mitume 13:6-12

6 Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;

7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.

8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.

9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,

10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?

11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.

12 Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.

Roho mtakatifu msaada wetu.

Jumatano jioni tuliona jinsi ambavyo Barnaba na Sauli waliwekwa wakfu kwa utume kwa maelekezo ya Roho Mtakatifu. Somo la asubuhi hii ni mwendelezo wa somo hilo la Jumatano, ambapo Barnaba na Sauli katika kuhubiri Injili, mchawi aliyetaka kushindana nao alikuwa kipofu.

Barnaba na Sauli waliitwa kwa maelekezo ya Roho Mtakatifu. Waliitenda kazi kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu.

Kumbe nasi tunayo nafasi ya kutumika kama wao, maana tumempokea Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu. Tuitende kazi ya Mungu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliye msaada wetu.

Siku njema.

 

Heri Buberwa