Date: 
01-06-2023
Reading: 
Matendo ya mitume 4:27-31

Hii ni Pentekoste 

Alhamisi asubuhi tarehe 01.06.2023

Matendo ya Mitume 4:27-31

27 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,

28 ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee.

29 Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote,

30 ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.

31 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.

Roho Mtakatifu msaada wetu;

Katika sura ya 3, Petro na Yohana walikuwa wakikwea hekaluni kusali, na kwenye lango la hekalu wakamwombea uponyaji kiwete. Mji ulitaharuki, wakawekwa gerezani. Hata asubuhi walipohijiwa, walibaki na msimamo wa kuhubiri Injili.

Walipoachiwa na baraza wakaendelea kuhubiri, na katika kuhubiri kwao mstari wa 31 unaonesha watu wakijawa Roho Mtakatifu na kuendelea kunena habari za Yesu kwa ujasiri.

Petro na Yohana walinena kwa ujasiri kwa sababu ya nguvu ya Roho Mtakatifu. Nasi tunaweza kuishi tukimpendeza Mungu kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Siku njema.

 

Heri Buberwa