Date: 
31-05-2023
Reading: 
Yohana 6:43-46

Hii ni Pentekoste

Jumatano asubuhi tarehe 31.05.2023

Yohana 6:43-46

43 Basi Yesu akajibu, akawaambia, Msinung'unike ninyi kwa ninyi.

44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.

45 Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu.

46 Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba.

Roho mtakatifu msaada wetu.

Katika sura ya 6 ya Injili ya Yohana, Yesu anawalisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili. Baada ya hapo Yesu anajitambulisha kama chakula chakula cha uzima, kilichoshuka toka mbinguni. Ndipo Wayahudi wananung'unika kwa sababu Yesu alisema ametoka mbinguni.

Sasa somo la asubuhi hii Yesu anawaambia wasinung'unike maana hakuna awezaye kumwendea bila kuvutwa na Baba. Yesu alikuwa anawaambia kumfuata yeye aliyeshuka toka mbinguni. Ujumbe huu unatujia sisi asubuhi hii, kwamba tumwendee Yesu aliyeshuka toka mbinguni. Tunadumu katika Kristo kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Siku njema.

 

Heri Buberwa