Date: 
24-05-2023
Reading: 
Yohana 7:37-40

Jumatano asubuhi tarehe 24.05.2023

Yohana 7:37-40

37 Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.

38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.

40 Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.

Usikie kuomba kwetu;

Sura ya saba ya Injili ya Yohana inaonesha kwamba pamoja na Yesu kuhubiri na kufundisha, bado wapo watu ambao hawakumuamini wakiwemo ndugu zake. Mstari wa 5 unadhihirisha hili;

Yohana 7:5
Maana hata nduguze hawakumwamini.

Lakini katikati ya kutokuaminika, tunaona Yesu akisimama na kusema mtu akiona kiu na aje kwangu. Anaita waliomsikiliza kumuamini. Sisi tuendelee kumwamini Yesu kama tulivyompokea tukidumu katika sala maana yeye husikia kuomba kwetu.

Siku njema.

 

Heri Buberwa