Date: 
13-03-2021
Reading: 
Mwanzo 1:9-13 (Genesis 1:9-13)

JUMAMOSI TAREHE 13 MACHI 2021, ASUBUHI

MWANZO 1:9-13

 9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.
10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.

Tuulinde uumbaji;

Ni siku ya tatu ya uumbaji, ambapo Mungu anafanya maji na kuyaita bahari. Anatenganisha bahari na nchi kavu. Anaotesha majani na miti izaayo matunda.

Ni udhihirisho wa ukuu wa Mungu katika uumbaji. Ni wazi Mungu ndiye muumbaji, na ndiye anayeamuru kila kitu. Anatuamuru kulinda vitu vyote  alivyoviumba, ili dunia iendelee kuwa mahali salama pa kuishi, kwa viumbe vyote. Linda uumbaji.

Jumamosi njema.


SATURDAY 13TH MARCH 2021, MORNING

Genesis 1:9-13 New International Version

And God said, “Let the water under the sky be gathered to one place, and let dry ground appear.” And it was so. 10 God called the dry ground “land,” and the gathered waters he called “seas.” And God saw that it was good.

11 Then God said, “Let the land produce vegetation: seed-bearing plants and trees on the land that bear fruit with seed in it, according to their various kinds.” And it was so. 12 The land produced vegetation: plants bearing seed according to their kinds and trees bearing fruit with seed in it according to their kinds. And God saw that it was good. 13 And there was evening, and there was morning—the third day.

It is the third day of creation, where God makes water and calls it the sea. He separates the sea from dry land. He grows leaves and trees that bring forth fruit.

It is a manifestation of God's greatness in creation. Obviously God is the creator, and he commands everything. He commands us to defend all things He has created, that the earth may remain a safe place to live, to all creation. Protect creation.

Good Saturday.