Date: 
22-03-2022
Reading: 
Mwanzo 1:6-8

Hii ni Kwaresma 

Jumanne asubuhi tarehe 22.03.2022

Mwanzo 1:6-8

6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji.

7 Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.

8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.

Tutunze uumbaji;

Ni siku ya pili Mungu akiendelea na uumbaji, ambapo tunasoma akitenga maji yaliyo juu na chini na kufanya anga, akiliita anga hilo mbingu. 

Mungu alikuwa akiendelea na mpango wa kumpatia makazi mema, mazuri na ya kudumu, mwanadamu aliyekuja kumuumba. Ni kwa jinsi gani tunaitunza dunia hii aliyoiumba Mungu na kutufanya tuishi humo? 

Tunayo nafasi ya kudumisha kazi ya Mungu kwa kutunza uumbaji wake. Unatimiza wajibu wako katika hili?

Siku njema