PICHA NA HABARI ZA MTAA WA TABORA UNAOTUNZWA NA AZANIAFRONT

Mchungaji Prudence Chuwa akiendesha Ibada ya Ubatizo katika mtaa wa Tabora . Mtaa huu una jumla ya washarika 20

Washarika katika mtaa wa Tabora wakifuatilia Ibada iliyoendeshwa na Mchungaji Prudence Chuwa kutoka Usharika wa Knisa Kuu, Azaniafront. Ibada hiyo ilifanyika tarehe 19/08/2018. Picha na Paulin Paul/AZF

Mchungaji Prudence Chuwa akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la kudumu la Kanisa. Washarika katika mtaa huu wa Tabora wamekuwa wakilazimika kuhairisha ibada katika msimu wa mvua kutokana na jengo wanalolitumia kwa sasa kutokuwa na uimara wa kutosha. Picha na Paulin Paul/AZF

Picha ya pamoja; Mchungaji Prudence Chuwa akiwa na washarika wa mtaa wa Tabora muda mfupi mara baada ya Ibada katika mtaa huu kumalizika. Picha na Paulin Paul/AZF

Washarika katika mtaa wa Tabora wakiwa wamesimama kuashiria kuanza kwa ibada iliyoongozwa na Mchungaji Prudence Chuwa kutoka Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront akisaidiana na Mtumishi Onesmo Uroki wa mtaa huu wa Tabora. Picha na Paulin Paul/AZF