Date: 
04-09-2021
Reading: 
Mithali 25:21

Jumamosi asubuhi 04.09.2021

Mithali 25:21

[21]Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; 

Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa;

Tuwapende jirani zetu;

Inajulikana kuwa ili mtu aishi anahitaji vitu vitatu; Chakula, Hewa na Kinywaji. Bila hivyo vitu mtu hufa mara moja. Katika njia tofauti za maisha, mtu huweza kukosa mahitaji muhimu kama chakula na maji ili aweze kuishi.

Kuishi ni haki ya kila mtu aliyeumbwa na Mungu. Ndiyo maana tunaagizwa kuwapa chakula adui zetu ili waishi. Mtu asife kwa kukosa chakula kwa sababu ni adui yako!

Kwa tafsiri pana, tunapotoa huduma na(au) kusaidiana, tusibaguane. Tuhudumiane kwa upendo, kama watoto wa Baba mmoja, Yesu Kristo aliye mwokozi wetu. Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Jumamosi njema.