Date: 
23-04-2021
Reading: 
Micah 7:14-17

FRIDAY 23rd  APRIL 2021 MORNING                                       

Micah 7:14-17 New International Version (NIV)

14 Shepherd your people with your staff,
    the flock of your inheritance,
which lives by itself in a forest,
    in fertile pasturelands.[a]
Let them feed in Bashan and Gilead
    as in days long ago.

15 “As in the days when you came out of Egypt,
    I will show them my wonders.”

16 Nations will see and be ashamed,
    deprived of all their power.
They will put their hands over their mouths
    and their ears will become deaf.
17 They will lick dust like a snake,
    like creatures that crawl on the ground.
They will come trembling out of their dens;
    they will turn in fear to the Lord our God
    and will be afraid of you.

Dear brothers and sisters in Christ, we must never forget the faithfulness of the Lord.  Even when we are faithless, He cannot deny who He is.  He is the Holy, Faithful, and Righteous One. The punishment for our sins and the trials that sharpen our faith are so temporary when compared to God’s care of our lives. 

Apostle Paul told Timothy that, “If we endure, we will also reign with him. If we disown him, he will also disown us; if we are faithless, he remains faithful, for he cannot disown himself” (2 Timothy 2:12–13).


IJUMAA TAREHE 23 APRILI 2021  ASUBUHI                          

MIKA 7:14-17

14 Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, mwituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.
15 Kama katika siku zile za kutoka kwako katika nchi ya Misri nitamwonyesha mambo ya ajabu.
16 Mataifa wataona, na kuzitahayarikia nguvu zao zote; wataweka mikono yao juu ya vinywa vyao, masikio yao yatakuwa na uziwi.
17 Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa Bwana, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.

Ndugu zangu wapendwa katika Kristo, hatupaswi kusahau uaminifu wa Mungu.  Hata pale tunapokosa kuwa na imani, yeye atabaki kuwa Mungu.  Yeye ni mtakatifu, mwaminifu, na mwenye haki. Adhabu ya maovu yetu na majaribu yanayoimarisha imani yetu ni ya muda tu ikiwa tutayalinganisha na jinsi Mungu anavyojishughulisha na maisha yetu.  

Mtume Paulo alimwandikia Timotheo kuwa, Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi;
13 Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.”
 (2 Timotheo 2:12–13).