Date: 
26-03-2022
Reading: 
Mhubiri 11:6

Hii ni Kwaresma 

Jumamosi asubuhi tarehe 26.03.2022

Mhubiri 11:6

Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa,kama ni hii au hii,au kama zote zitafaa sawasawa.

Tutunze uumbaji;

Tunasoma juu ya kupanda mbegu, kwa maana pana ya kutumia uumbaji wa Mungu kwa ajili ya mahitaji na maendeleo yetu. Kutojua ipi mbegu ni sahihi, na kutozuia mkono wako, ni kuwa na bidii katika kutumia uumbaji wa Mungu yaani nchi, ili kujipatia riziki.

Tunaalikwa kufanya kazi kwa bidii, tukitumia uumbaji wa Mungu katika kazi zetu ili tuweze kuishi. Kwa maana nyingine, uumbaji wa Mungu ni zawadi kwetu ili tuweze kuishi bila kuwa tegemezi. Jambo kubwa na muhimu ni kutumia uumbaji huu kwa njia sahihi, na kwa utukufu wa Mungu.

Siku njema.