Date: 
18-04-2020
Reading: 
Matthew 28:11-15

SATURDAY 18TH APRIL 2020   MORNING                                              

Matthew 28:11-15 New International Version (NIV)

11 While the women were on their way, some of the guards went into the city and reported to the chief priests everything that had happened. 12 When the chief priests had met with the elders and devised a plan, they gave the soldiers a large sum of money, 13 telling them, “You are to say, ‘His disciples came during the night and stole him away while we were asleep.’ 14 If this report gets to the governor, we will satisfy him and keep you out of trouble.” 15 So the soldiers took the money and did as they were instructed. And this story has been widely circulated among the Jews to this very day.

The greatest event in the history of the world and of the faith people was the bodily resurrection of the Lord Jesus Christ, yet the vast majority of the world refuses to believe it.

Dear fellow Christians, don’t give up on your loved ones. Don’t give up on your neighbors. Keep praying for them, keep living out your faith and keep sharing the gospel on them. Look for opportunities to plant a little seed in the middle of a conversation. We do not need to come out with various tricks to make them believe, it is God’s work.

Relax in the great sovereignty of God and watch what He does as He penetrates hearts that are dead and blind and veiled because of their unbelief.


JUMAMOSI TAREHE 18 APRILI 2020  ASUBUHI                                

MATHAYO 28:11-15

11 Nao wale walipokuwa wakienda, tazama, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha wakuu wa makuhani habari za mambo yote yaliyotendeka.
12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi,
13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala.
14 Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.
15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.

Tukio kubwa kuliko yote katika historia ya dunia na ya watu wenye imani lilikuwa ni lile la kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Hata hivyo, watu wengi hawasadiki jambo hili.

Wapendwa Wakristo wenzangu, usichoke kuwahubiria wapendwa wako. Usikate tamaa juu ya maisha ya jirani yako. Endelea kuwaombea, endelea kuishi imani yako na kuwashirikisha habari njema za Ufalme wa Mungu. Tafuta fursa ya kupanda angalau mbegu ndogo katikati ya mazungumzo yenu. Hatuhitaji kubuni mbinu tofauti za kuwafanya waamini, hivyo ni kazi ya Mungu mwenyewe.

Tulia katika ukuu wa Mungu, nawe utaona jinsi atakavyotenda kwa kupenya katika mioyo iliyopofushwa na kufa kwa ajili ya kutokuamini kwao.