Date: 
05-03-2021
Reading: 
Mathayo 7:24-27

IJUMAA TAREHE 5 MACHI 2021
Mathayo 7:24-27


Wajenzi wenye hekima na wajenzi wapumbavu


24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

Ujumbe mkuu kwa Mkristo siyo tu kumwalika Yesu kukaa moyoni mwake; na kwamba kila kitu kitakwenda sawa na rahisi tangu siku hiyo.

Kila mmoja wetu anakumbana na “mvua, mafuriko na pepo” katika maisha yake: wale waliojenga maisha yao juu ya mwamba na hata wale waliojenga maisha yao juu ya mchanga.

Tofauti siyo kwamba ukiwa Mkristo hukutani na dhoruba; tofauti ni kwamba kuwa Mkristo unao msingi imara unaokulinda dhidi ya dhoruba.

 



FRIDAY 5TH MARCH 2021


Mathew 7:24-27

The Wise and Foolish Builders


24 “Therefore everyone who hears these words of mine and puts them into practice is like a wise man who built his house on the rock. 25 The rain came down, the streams rose, and the winds blew and beat against that house; yet it did not fall, because it had its foundation on the rock. 26 But everyone who hears these words of mine and does not put them into practice is like a foolish man who built his house on sand. 27 The rain came down, the streams rose, and the winds blew and beat against that house, and it fell with a great crash.”

The message of Christianity is not just ask Jesus into your heart and everything will be smooth and easy from this day forward.

There is “rain and floods and wind” for everyone in this life: those who build their life on the rock, as well as for those who build their life on the sand.

The difference is not that you don’t have storms as a Christian; the difference is that as a Christian you have a foundation that holds you up through the storms.